Karibu kwenye Sensa ya Mwaka 2011
Jumapili tarehe 10 Mwezi Aprili, mwezi wa nne. Sensa ya kina ya kuhesabia watu itafanyika hapa Ireland. Sensa hii itamuhesabia kila mtu ambaye atakuwepo Ireland usiku huo. Taarifa ya idadi na takwimu za watu ni kwa ajili ya matumizi ya takwimu na hesabu tu na itapatikana kwa mtu yeyote kwa kuitumia. Matokeo ya kwanza ya kuhesabia huku kwa watu yatapatikana mwezi wa saba mwaka huu.
Tafadhali bonyeza maelekezo hapo chini kwa habari zaidi kuhusu Sensa ya mwaka 2011.
Angalia/pakua fomu iliyofafsiriwa.
Angalia /Pakua Kitabu kidogo au kipeperushi cha maelekezo ya Sensa.
Angalia/Pakua Taarifa na Ripoti ya sensa ya mwaka 2006 kuhusu “Watu wa mataifa mengine wanaoishi hapa Ireland” (Kwa Kiingereza tu.
Habari kuhusu Sensa ya mwaka ya mwaka 2011
Sensa nini?
Sensa ni hesabu ya watu wote waliopo hapa katika nchi hii usiku wa sensa. Usiku wa sensa, kila mmoja aliye hapa katika nchi hii lazima ajazwe kwenye fomu ya sensa ili awe sehemu ya hesabu rasmi ya watu na makazi ambayo inafanyika kila baada ya miaka mitano hapa Ireland.
Sensa inayofuata itafanyika lini?
Sensa inayofuata itafanyika Jumapili tarehe 10 mwezi Aprili, mwezi wa nne mwaka huu 2011. kila mmoja aliye hapa katika nchi hii tahehe hiyo lazima ajazwe kwenye fomu ya sensa. Lazima uhesabiwe katika sensa hii popote ulipo hapa Ireland. Uwe upo nyiumbani, au upo kuwatembelea ndugu na jamaa na marafiki au hata hospitali, na kadhalika.
Je ni lazima nijaze fomu?
Ndiyo, kila mmoja aliye hapa katika nchi usiku wa sensa hii lazima ahesabiwe. Hii ni kwa mujibu wa sheria. Taarifa zinazokusanywa katika sensa ni muhimu kwa mipango yenye faida na manufaa kwetu sote,ndiyo maana ni muhimu sana kila mmoja kuhesabiwa.
Ni nini natakiwa kufanya?
Muhesabiaji wako ataleta fomu ya sensa katika makazi yako wiki tatu 3 mpaka nne 4 kabla ya usiku wa sensa tarehe 10 mwezi Aprili, mwezi wa nne. Iweke na uitunze fomu hii mahali pa usalama mpaka siku ya sensa. Muhesabiaji wako atafurahi na atakuwa tayari kujibu maswali yoyote utakayo kuwa nayo kuhusu fomu.
Siku ya sensa jaza fomu ya sensa kwa kumjaza kila mtu katika kaya yako na piga sahihi tamko la kiapo mwisho wa fomu ukishamaliza. Muhesabiaji wako atakuja tena ndani ya wiki mbili 2 au tatu 3 baada ya siku ya sensa kukusanya fomu yako. Atafurahi na ataweza kukusaidia wewe kama umekuwa na shida au tatizo lolote kuijaza fomu. Unaweza kuangalia kitambulisho cha muhesabiaji kwa kumwomba uangalie kitambulisho chake cha kuwa ya ni muhesabiaji wa sensa.
Je ni siri?
Ndiyo, majibu yote unayotoa na kujaza katika fomu ya sensa ni siri kabisa na yatatumika tu kwa ajili ya takwimu na hesabu za watu. Hakuna taarifa yoyote binafsi uliotoa itapelekwa kwenye kitengo au taasisi nyingine au idara na wizara ya serikali. Hii inalindwa na sheria.
Sensa inatumika kufanya nini?
Sensa inatumika kutoa habari za hesabu kuhusu watu wote wanokaa hapa Ireland. Habari hizi zinatumika na serikali, mikoa na tawala za mitaa, biashara na jumuia za mahali na nyinginezo kusaidia katika kufanya maamuzi kuhusu mipango ya elimu, afya, kazi, usafiri na hudumu nyingine nyingi. Taarifa zinazotolewa hazionyeshi mambo ya binafsi ya mtu. Bonyeza hapa kwa habari zaidi kwa kiingereza juu ya faida za sensa.
Wapi naweza kupata msaada?
Muhesabiaji wako afurahi na atakuwa tayari kujibu maswali yoyote utakayo kuwa nayo kuhusu sensa au kujaza fomu ya sensa.
Tafsiri ya fomu hii inapatikana katika lugha ishirini na moja 21 zifuatazo: Kipolishi, Kirumenia, Kiluthuania, Kifaransa, Kijerumani, Kirusi, Kiispania, Kiyoruba, Kichina, Kislovakia, Kihangari, Kireno, Kiarabu, Kiitaliano, Kicheki, Kilativia, Kiestonia, Kibulgaria, Kihindi, Kiurdu, Kiswahili. Unaweza kuona taarifa katika kila moja ya lugha hizi kwa kubonyeza hapa.
Unaweza bonyeza katika maelezo hapo chini kupata taarifa zaidi kuhusu fomu ya sensa na jinsi ya kuijaza katika kiingereza.
Kwa hiyo jaza fomu yako ya sensa Jumapili, tarehe 10 mwezi Aprili, mwezi wa nne na usaidie kuifanya sensa ya mwaka 2011 iwe ya mafanikio.